Schools
Services Provided
Project Year
Project Overview
Asasi (NGO) ya the Struggle for Community Support Alliance (SCSA) au Pambana Saidia Jamii iliyosajiliwa kwa ngazi ya Taifa imefunga mwaka 2013 wilayani Kyela ambako shughuli zake huanzia na kusambaa nchi nzima. Nikiwa Mwenyekiti Mtendaji wa NGO hii nimeshiriki kufunga mwaka kwa kutoa misaada mbalimbali kama vile mifuko 133 ya saruji na mabati kwenye shule za msingi wilayani Kyela ambazo ni Isaki, Lubele, Ngamnga, Itenya, Butangali, Lukama, Mababu na Matema. Aidha, NGO hii imetoa vifaa vya michezo kama vile jezi, mipira na nyavu kwa timu 6. Vilevile Pambana Saidia Jamii imetoa fedha kwa vikundi vya ujasiriamali Ikolo, Ipyana na Matema. NGO hii pia imetoa nondo na suruji kwaajili ya ujenzi wa kidaraja mtaa wa Ipyana B. Mwaka 2014 tutatekeleza mradi wa majaribio (Pilot Project) wa gesi hai (Biogas) kwa kujenga mitambo (Biogas Compact Plants) ipatayo 40 angalau mitambo 2 kwa kila kata zote 20 wilayani Kyela. Mradi huu ukikamilika utasaidia kupata nishati mbadala ya kupikia, mbolea mashambani, kupunguza ukataji miti hovyo na kuokoa muda wa kutafuta kuni hususan kwa wanawake na watoto
